Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 23, 2012

Nape akutana na Ujumbe wa Wanafunzi kutoka Marekani jijini Dar


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akizungumza wakati wa kikao chake na Ujumbe wa wanafunzi kutoka Marekani waliotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, leo. Nape alijadili nao masuala mbalimbali ya siasa. Kushoto ni Kiongozi wa msafara huo, Jola Yoder kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, Marekani.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akimkabidhi 'opener' za CCM Mkuu wa msafara wa Ujumbe wa wanafunzi kutoka Marekani, Jola Yoder kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Spokane, Marekani, baada ya mazungumzao na ujumbe huo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, leo.
Nape akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Marekani waliofika Ofisi ya Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...