Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 24, 2012

FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA KUPAMBANA TENA SIKU YA SABASABA

Francis Cheka na Japhet Kaseba uso kwa uso siku ya sabasabaNa Mwandishi Wetu

BINGWA wa kick Boxing. Japhet  Kaseba amesaini mkataba wa kucheza na
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano

;Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke lakini awajui mimi ni bingwa katika mapigano yote alisema Kaseba;


Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na kukata ngebe za cheka ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli bingwa wa kweli ni Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu mpaka sasa cheka kanikimbia mda mrefu tu tangia tupambane 3 October 2009  ambapo alipewa ubingwa kwa kusingizia mshabiki wangu alikuja kumtupa nje ya uwanja kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika,

Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi


Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;

1 comment:

  1. that good big match champion kickboxing vs champion boxing you thing who winner ?

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...