Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 26, 2012

COCACOLA YAZINDUA KAMPENI YA SABABU BILIONI ZA KUITHAMINI AFRIKA)Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Filbert Bayi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya sababu bilioni za kulithamini bara la Africa iliyoandaliwa na Kampuni ya Cocacola ambapo Bayi alisema kuwa kuna haja ya watanzania kuonyesha uzalendo wa nchi yao na kuithamini Africa, Uzinduzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City uliopo jiini Dar es Salaam.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Meneja mkazi wa masoko kampuni ya Cocacola Bw. Dimej Olaniyan akifafanua kuhusu kampeni hiyo ambapo alisema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa miaka miwili na inalengo la kuinua yale mazuri yanayo onekana katika bara la Afrika.
Meneja wa masoko kampuni ya Cocacola Bi.Salome Mabirizi akielezea muhimu wa kuwa na Kampeni hiyo.
Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Filbert Bayi Pamoja na)Meneja mkazi wa masoko kampuni ya Cocacola Bw. Dimej Olaniyan wakipata kiburuisho cha soda ya Coca cola.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika kampeni hiyo.
Mmoja wa waandishi wa habari kutoka katika Gazeti la Mwananchi (katikati) Nora Damian aliyejinyakulia zawadi ya Televisheni akikabidhiwa zawadi yake na Meneja mkazi wa masoko kampuni ya Cocacola Bw. Dimej Olaniyan (kulia) kushoto ni Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Filbert Bayi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...