Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 29, 2012

SIMBA KUIVAA AL AHLY SHANDY YA SUDAN LEO UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.


Wawakilishi pekee waliobaki toka Klabu za Tanzania katika michuano ya Barani Afrika, Simba, leo wanatinga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Al Ahly Shandy ya Sudan.

Katika Raundi zilizopita, Simba walibwaga Kiyovu ya Rwanda kwa jumla mabao 3-2 katika Mechi mbili kisha kuwatoa ES Setif ya Algeria kwa bao la ugenini baada ya kufungana bao 3-3 katika Mechi mbili, Simba wakishinda Dar es Salaam bao 2-0 na kuchapwa 3-1 huko Mjini Setif, Algeria.

Nao Al Ahly Shandy waliwatoa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji Raundi iliyopita na ingawa Klabu hii ya Sudan ni mara ya kwanza kucheza michuano ya Klabu Afrika lakini kwa mchezo ilioonyesha walipocheza na Ferroviario de Maputo na kushinda 1-0 ugenini Maputo na 2-0 kwenye Mechi ya marudiano, Timu hii si ya kubeza.

Timu hizi zitarudiana hapo Jumamosi Mei 12 huko Mjini Shandy, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

Na katika mechi hiyo kiingilio cha chini ni sh 5,000/=

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...