Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 4, 2014

AZAM FC YAPATA UDHAMINI WA BENKI YA NMB

 

Na Fadha Kidevu Blog
MABINGWA wa soka Tanzania bara wameingia mkataba wa miaka miwili na Benki ya NMB  jana
Kwa mujibu wa Mweyekiti wa Azam Said Mohamed alisema mkataba huo utakuwa ikiisadia timu hiyo mambo mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo kama Jezi,Viatu na nauli ya kusafiria wakati wa mechi za mikoani.
 
“Udhamini wetu na NMB,utakuwa  ukihusisha vifaa vyote vya michezo ikiwemo Jezi,Viatu na vifaa vingine na hatuwezi kusema gharama yake kwa sababu ni makubaliano yetu sisi na NMB ,”alisema Mohamed.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Mark Wiessing alisema mafanikio ya Azam FC pamoja na uongozi bora ndivyo vilivyo wavutia kuingia nao mkataba huo ambao anaamini utakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
 
Hiyo siyo mara ya kwanza kwa NMB kujiingiza katika udhamini wa michezo mara ya kwanza iliwahi kuidhamini timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,mwaka 2007 hadi 2010 na imekuwa ikitoa mchango katika kuendeleza soka la vijana nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...