Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 29, 2014

Mh. Lowassa amkaribisha Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh.  Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo jana Jumapili Septemba  28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya  kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.
Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha  Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni  kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli,Bw. Twalib  Mbasha.
Balozi wa Japan nchini,Mh. Masaki Okada (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha (kulia) na Meneja wa  Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema alikofikia balozi huyo na 
ujumbe wake katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...