Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 5, 2014

MWANAAFA MWINZAGO ATEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS.


Mwanaafa Mwinzago akipozi katika studio za Global TV Online.
Staa wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwizago kutoka Kanda ya Kusini Mkoa wa Mtwara akiwa ndani ya Studio za Kampuni ya Global Publishers Ltd wakati alipokwenda kufanyiwa Mahojiano na Wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikiendi.
 Mara baada ya Kutua katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ambao ni Wachapishaji wa Magazeti Pendwa Hapa Nchini Mwanaafa alipata nafasi ya Kuongelea Namna ya Yeye alivyoweza Kuibuka Mshindi katika Shindano hilo Kubwa na La Kwanza Kufanyika Afrika Mashariki na Kati lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) huku akielezea Jinsi alivyoweza kupokea ushindi alioupata Mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Ambapo Fainali ya Shindano hilo Kubwa ilipofanyika na Yeye Kuibuka Kinara wa Shindano hilo kwa Mara ya Kwanza.
Shindano La Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano la Kwanza na Kubwa Kufanyika kwa mara ya Kwanza Afrika MAshariki na Kati huku likiwa limejinyakulia Sifa na Umaarufu wa Hali ya Juu kutokana na Umahiri wa Uendeshaji wa Shindnao hilo ambapo Watanzania Wengi wamefurahishwa na Uendeshaji wake uliojikita katika Utendaji wa Haki ambapo Mshindi alipatikana kihalali.
Tanzania Movie Talents (TMT) imepelekea sasa kuwafanya baadhi ya Watanzania ambao waliokuwa wanajua kuwa shindano hili halitatenda haki basi Kuanzia sasa wamejionea kuwa TMT ipo kwaajili ya kutoa haki. TMT ni shindano ambalo  kiukweli Limefungua Njia Kwa Watanznaia Ambao wana vipaji lakini hawajapata nafasi ya Kuonekana.
Tanzania Movie Talents (TMT) limeendeshwa takribani Miezi Minne huku kukiwa na Changamoto Nyingi ambazo timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambayo ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano hili Kubwa kujitahidi kutatua changamoto hizo ili kuhakikisha Shindano hilo linafanyika kwa Ustadi wa hali ya Juu na Utofauti.
Mbali na Zawadi hiyo kubwa aliyoshinda Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwizago zawadi nyingine ambayo amepata Kutoka Kampuni ya Proin Promotions ni Kuwa Kampuni ya Proin itamsomesha Mwanaafa Mwizago katika Level Zote kwasababu kampuni inatambua Umuhimu wa Elimu Kwa Mtanzania.
Sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limemalizika kwa Mshindi mmoja wapo kutoka kanda ya Kusini Mkoa wa Mtwara Mwanaafa Mwizago kuibuka Kidedea na Kujinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washiriki wengi wote tisa waliofanikiwa kuingia hatua ya Fainali wakisubiri kucheza filamu ya Pamoja ambapo filamu hiyo itauzwa na Kusambazwa na Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu Tanzania ya Proin Promotions Ltd.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...