Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 17, 2014

FILAMU KUTOKA PROIN PROMOTIONS LIMITED ZAFANIKIWA KUPITA MCHUJO WA KUONYESHWA KATIKA TAMASHA LA ARUSHA FILM FESTIVAL 2014


Kava la Filamu ya KITENDAWILI iliyochezwa na Single Mtambalike au Rich Rich, Irene Veda na Haji Adam ambayo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited
Kava la Filamu ya NETWORK iliyochezwa na MONALISA NA BRIAN ambayo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.


Tamasha la Arusha Film Festival ni tamasha la kimataifa ambalo linatarajiwa kufanyika kwa Mara ya Tatu mfululizo, ambapo litaanza tarehe 20 mpaka 27 Mwezi wa tisa (september) Jijini Arusha.


Arusha Film Festival 2014 tayari imeshatangaza majina ya filamu zilizochaguliwa kuonyeshwa katika tamasha hilo kubwa la kimataifa ambalo hujumuisha filamu toka mabara yote yaani Africa, Ulaya, Marekani na Asia. 

Filamu zilizochaguliwa kuingia katika Tamasha hizo kutoka kampuni mahiri ya utengenezaji na usambazaji wa filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited na ambazo zina ubora wa kimataifa huku filamu hizo kutoka Proin Promotions ltd zikiiwakilisha vyema Tanzania. 
Filamu zilizoingia katika tamasha hilo na  zenye ubora wa Kimataifa kutoka Kampuni ya Proin Promotions Ltd ni pamoja na Kitendawili(feature), Kigodoro(Feature), Sunshine(Feature), Network(Feature).
Filamu hizi za Kitanzania zina sehemu moja tu yaani part 1 na sio Part 1 na part 2. Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya filamu kuwa Na Sehemu Moja tu yaani Part 1 ndio sababu filamu kutoka Proin Promotions zimefanikiwa kupita mchujo ambapo Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambayo haitaki part 1 na part 2 kwa lengo la  kukuza tasnia ya filamu nchini.
Filamu za Tanzania zenye part 1 na part 2 zimetupwa nje sababu waandaji na wataalamu wa nje wameziona hazina ubora wa muda katika standard ya kimataifa na vigezo  vinginevyo.
Filamu hizo za Tanzania zitaonyeshwa pamoja na filamu mbalimbali nyingine zilizopita katika mchujo huo toka mataifa mabalimbali ikiwemo Canada, Kenya, Uganda, Austalia, Rwanda, Spain, S.Africa, Guinea Bisau, Brazil, Nigeria, Switzerland, Argentina, UK, Burundi, Morocco. Ili kuona List nzima ya filamu hizo ingia hapa Selected Films Arusha Film Festival 2014.
Vilevile kutakuwa na zoezi la utoaji wa tuzo  katika tamasha hilo la filamu kwa kazi nzuri.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...