Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 23, 2014

Kajala kuzindua Mbwa Mwitu kesho Mlimani City


Kajala katika pozi
Kava la picha hiyo ya Mbwa Mwitu inayozinduliwa kesho Mlimani
NYOTA wa filamu nchini Kajala Masanja 'Kajala' kupitia kampuni yake ya Kay Entertainment inatarajiwa kuzindua filamu ya aina yake kesho usiku.
Filamu hiyo inayofahamika kama 'Mbwa Mwitu' itazinduliwa kwenye ukumbi wa Mlimani City kwa watu maalum walioalikwa kuhudhuria.
Kinachoifanya filamu hiyo kuwa ya kipekee ni muda mfupi iliyonayo wa dakika 15 tu, 10 ikiwa ni filamu yenyewe na tano za 'ducumentary' ya baadhi ya vijana waliokuwa wakiunda kundi la Mbwa Mwitu lililotikisa jiji.
Mtunzi na muongozaji wa filamu hiyo, Leah Richard 'Lamata' aliiambia MICHARAZO kuwa, filamu hiyo inasimulia visa na mikasa ya kundi la Mbwa Mwitu lililohusishwa na uvamizi na uporaji wa watu jijini Dar es Salaam.
"Uzinduzi utafanyika Mlimani Sept 24 (kesho) na ndani ya filamu hiyo ya dakika 10 ina nyongeza ya dakika tano za mahojiano ya waliokuwa vijana wa 'Mbwa Mwitu' ambao wameacha uhalifu huo," alisema Lamata kwa niaba ya Kajala ambaye ni mmoja wa washiriki wa filamu hiyo.
Mbali na Kajala wengine walioicheza ni Hemed Suleiman 'PHD', Grace Mapunda 'Mama Kawele', Mwinjuma Muumin, Abort Rocca, Hassain Hussein na Abdul Karim.
Kundi la Mbwa Mwitu na yake ya Watoto wa Mbwa, Boda kwa Boda na Bad Face yalitikisa jiji kwa vitendo vyao ya kihalifu kabla ya jeshi la Polisi kuyashughulikia huku baadhi ya washirika wao kuuwawa na wananchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...