Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 15, 2014

YANGA KUANZA KUJINOA KESHO TAYARI KWA KUIVAA MTIBWA SUGER


Na Father Kidevu Blog
KIKOSI cha Yanga kesho kinatarajia kuendelea na maandalizi ya Ligi Kuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, na Alhamisi itasafiri kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kwenye uwanja wa Jamuhuri Jumamosi.

Washindi hao wa mchezo wa Ngao ya Jamii leo wamepumzika baada ya jana kutoa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya bingwa wa msimu uliopita Azam kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mabao yaliofungwa na Geilson Santos ‘Jaja’ na Simon Msuva.

Meneja wa Yanga Hafidh Salehe,amesema katika kikosi kitakacho elekea Morogoro Alhamisi atakuwemo kiungo Mbrazili aliyekosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Andrey Coutinho,baada ya kupona maumivu hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...