Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 15, 2014

WASANII NYOTA NA WATU MAARUFU KUOSHA MAGARI SEPTEMBA 20 JUMAMOSI KATIKA VIAWANJA VYA BIAFRA JIJINI DAR
Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments, Ally Nchahaga (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare s Salaam jana, kuhusu tukio la uoshaji magari linalojulikana kama “Celebrities  Charity Car Wash” lenye lengo la kuchangia fedha Wodi ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, litakalowashirikisha watu maarufu wakiwemo wasanii nyota wa filamu nchini, litakalofanyika wakati wa Tamasha la Magari Auto Fest 2014, Septemba 20 mwaka huu katika Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar e s Salaam.  Kutoka (kushoto) ni Msanii nyota wa Bongofleva na Mkurugenzi wa Jaffarai Car Wash, Jaffai Msham, Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja na Msanii, Jenefer Kyaka ‘Odama’. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Msanii nyota wa Bongofleva na Mkurugenzi wa Jaffarai Car Wash, Jaffai Msham (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu ushiriki wake katika tukio la uoshaji magari linalojulikana kama “Celebrities  Charity Car Wash” lenye lengo la kuchangia fedha Wodi ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, litakalowashirikisha watu maarufu wakiwemo wasanii nyota wa filamu nchini, litakalofanyika wakati wa Tamasha la Magari Auto Fest 2014, Septemba 20 mwaka huu katika Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar.  Kutoka (wa pili kushoto) ni Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments, Ally Nchahaga , Msanii wa Bongo Movie, Jenefer Kyaka ‘Odama’ na Mratibu wa Tamasha, Fred Kimiti. 
Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare s Salaam jana, kuhusu ushiriki wake katika tukio la uoshaji magari linalojulikana kama “Celebrities  Charity Car Wash” lenye lengo la kuchangia fedha Wodi ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, litakalowashirikisha watu maarufu wakiwemo wasanii nyota wa filamu nchini, litakalofanyika wakati wa Tamasha la Magari Auto Fest 2014, Septemba 20 mwaka huu katika Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar.  Kutoka (kushoto) ni  Msanii nyota wa Bongofleva na Mkurugenzi wa Jaffarai Car Wash, Jaffai Msham, Msanii wa Bongo Movie, Jenefer Kyaka ‘Odama’ na Msanii Blandina Chagula ‘Johari’.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Dar es Salaam.
Masupa staa wa Tanzania wathibitisha ushiriki wao katika “Celebrities  Charity Car Wash” litakalo fanyika sambamba na tamasha la Auto Fest 2014. Linatarajiwa kufanyika tarehe 20th September, 2014 katika viwanja vya Biafra Kinondoni, Dar es Salaam.
                              
Waliosibitisha ushirki wao ni Irene Uwoya,Odama, Kajala Masanja, Monalisa, Aunty Ezekiel, Lulu Michael, Johari, JB, Ritchie.
Tamasha hili kwa mwaka huu litajumuisha “Celebrity Charity Car Wash” ikiwa ni njia moja wapo yakutoa hamasa kwa wananchi kuchangia wahanga wa ajali nchini. “Kutokana na matukio mengi ya ajali nchini tumeona nakutambua kuwa wengi wa majeruhi hutibiwa bure basi ni vyema tukaandaa tukio linalo husiana na tamasha letu wakati huo huo tukiweza kuchangia mahitaji muhimu katika wodi hizi”.  Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments. “Tunarajia watu watahamisika kukemea madereva wanao tumia barabara vibaya tukielekea katika wiki ya usalama barabarani.
Tukio hili linalenga kuchangisha fedha kwa mfumo wa kuosha magari kwa bei yakuafikiana na Supa staa “CELEBRITY”.  Tunakaribisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji huu. Lengo letu kwa mwaka huu likiwa nikuchangia Wodi ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Emergence Medicine Unit).
Burudani kwenye tukio zitahusisha,  Gari lililo pambwa (Pimped) ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao, Bingwa wa misele, Bingwa wa 4x4, B-Boy Dance, ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha magari kama norinda “misele”.
  
Tamasha la Autofest mwisho wa wiki linategemea kuvutia watu wengi, na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari Tanzania likiwa katika mwaka wake wa saba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...