Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 29, 2012

GARI LAMTOKEA PUANI MADA MAUGO BAPINGWA KWA K,O RAUNDI YA 7



 Bondia Francis Cheka (kulia) akimsukumia konde mpinzani wake Mada Maugo, wakati wa pambano lao lililokuwa la Raundi 12 lililofanyika katika Ukumbi wa PTA usiku huu. Mada Maugo aliwashangaza mashabiki wa mchezo huo pale alipoanza pambano hilo kwa spidi ya ajabu na kufanikiwa kumpeleka chini mpinzani wake mara mbili katika raundi ya pili na ya tatu, baada ya raundi ya nne mchezo ulibadilika na Mada kuanza kuelemewa na kupoteza mwelekeo huku akikumbatia kila mara.
Ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Mada Maugo alitangaza kutoendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi huku akisikika kusema, 'Sirudi Jamaa ataniua' huku akivua Glovz na kumpa ushindi mpinzani wake wa Teknical Know Count TKO.
Baada ya mchezo huo alipohojiwa na mtandao huu Mada alisema kuwa ilipofika raundi ya nne tu alikuwa hamuoni mpinzani wake jukwaani lakini alijikaza na kuendelea kushambulia huku akishtukia makonde yanatua usoni na ndipo ilipofika raundi ya sita aliamua kumwambia msimamizi wake kuwa hawezi kuendelea na pambano hilo.
 Mada Maugo, akimpeleka chini mpinzani wake Cheka.
 Mashabiki wa Mada, wakishangilia...
 Mada Maugo (kulia) akishambulia kwa konde zito.
 Wakichapana kwa zamu...
 Mada akishambulia....
 Mashabiki wa ngumi wakishangilia pambano hilo.
 Mashabiki wa Cheka, wakishangilia na kulizunguka gari alilokabidhiwa Cheka, baada ya kutangazwa mshindi.
 Cheka akisaidiwa na polisi baada ya kuzongwa na mashabiki wake wakitaka kumbeba na kuzunguka naye ukumbini humo baada ya kushinda pambano hilo.
 Nasib Ramadhan (kushoto) akichapana na Moro Best katika moja ya pambano la utangulizi, ambapo Nasib alishinda kwa KO katika Raundi ya nne.
 Simba wa Tunduru (kulia) akishangilia baada ya kumchapa mpinzani wake Mohamed Kashinde kwa KO katika Raundi ya 6 Dakika ya 2 na Sekunde 59, huku mohamed akiwa naongoza kwa mchezo bomba kabla ya kuangushwa.
 Simba wa Tunduru, akishangilia kwa staili yake baada ya kumwangusha mpinzani wake.
 Mgeni Rasmi, Meya wa Ilala, Jerry Slaa, akiwa na baadhi ya viongozi wa mchezo huo meza kuu wakifuatilia kwa makini mapambano hayo.
 Mrembo, Elizabeth Pertty, akipita jukwaani kuonyesha namba za raundi ya pambano hilo.
Cosmas Cheka (kulia) akipambana na Sadick Momba. Katika pambano hilo Momba alishinda kwa Pointi

4 comments:

  1. Excellеnt article! Wе are linking to
    thіѕ ρаrticularly great cοntent
    οn our ѕite. Keep up the great ωriting.


    Havе a look at my blog poѕt .
    .. http://quizilla.teennick.com

    ReplyDelete
  2. Wonderful work! This is the type of information that should
    be shared across the net. Disgrace on the seek engines for now not positioning
    this submit higher! Come on over and visit my web site .
    Thanks =)

    Also visit my site - nursing professor jobs san diego

    ReplyDelete
  3. I am no longer sure the place you are getting your info, however great topic.
    I needs to spend some time learning much more or working out
    more. Thanks for magnificent info I used to be searching for
    this info for my mission.

    Here is my web blog credit counseling yakima

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...