Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 11, 2014

FILIKUNJOMBE KUWALIPUA BUNGENI MAKANDARASI WABOVU LUDEWA , ASIFIA KAMPUNI YA BOIMANDA
 Mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto  akishirikiana na mwananchi wa  Lupingu  kukata  mti uliokuwepo katika njia ya kupitisha umeme  kutoka Ludewa kwenda  Lupingu baada ya mbunge huyo kushinda siku nzima  akishiriki maendeleo ya kupeleka umeme Lupingu jumla ya vijiji 49 Ludewa kupelekewa  umeme

Mbunge  Filikunjombe wa  pili  kulia akimsikiliza mwakilishi wa meneja wa Tanroads mkoa wa Njombe Bw  KIndole  wakati  akielezea maendeleo ya ujenzi wa barabara Ludewa 
...........................................................................................................................
MBUNGE  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amepania  kutumia dakika  zake 15  bungeni kuwalipua makandarasi wabovu  wanaoendelea na ujenzi wa barabara  mbali mbali katika wilaya ya Ludewa  ikiwemo barabara ya Njombe -Ludewa na Ludewa - Manda 

Mbunge  huyo alitoa kauli hiyo  juzi  wakati akikagua ujenzi wa barabara   hizo katika  wilaya ya  Njombe na  kuwa katika  baadhi ya maeneo hajafurahishwa na utendaji kazi wa kampuni  husika kutokana na kufanya  kazi hiyo  chini ya  kiwango na  kuwa  hadi sasa ni kampuni moja  pekee ambayo imeonyesha  kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...