Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 18, 2014

MWINA KADUGUDA AANDIKA KITABU CHA HISTORIA YA KLABU YA SIMBA, NA KUZINDULIWA NA WAZIRI MKAMIANaibu waziri wa habari, utamaduni na Michezo Juma Selemani Mkamia akikata utepe kwenye kitabu cha Historia ya klabu ya Simba ikiwa ni sehemu muhimu ya uzinduzi wa kitabu hicho kilicho tungwa na katibu wa zamani wa klabu hiyo Mwina Mohamed Kaduguda pichani Kulia
Naibu waziri wa habari, Vijana, utamaduni na Michezo Juma Nkamia amehudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu cha 'HISTORIA YA SIMBA'  kilichotungwa na kuandiskwa na mwandishi mkongwe wa habari hapa nchini ambaye pia ni katibu wa zamani wa klabu ya Simba Mwina Mohamed Kaduguda uzinduzi uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi.

Akitoa hotuba ya iliyo kuwa na historia ndefu ya klabu ya Simba, waziri Nkamia alitumia fursa hiyo kuwataka wanachama na mashabiki wa Simba kuwa kitu kimoja katika kipindi hiki kwa lengo la kuendeleza mambo mazuri na yenye mafanikio.

Nkamia amesema endapo wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo watashindwa kutimiza wajibu wao wa kuipenda klabu yao na kuithamini, kuna hatari kubwa ya kukosekana kwa historia nzuri kwa miaka ijayo.

Hata hivyo Nkamia amempongeza muandishi wa kitabu hicho Mwina Seif Mohamed Kaduguda kwa kutumia ujasiri wake kwa kuweka kumbukumbu mbayo katu haiwezi kufutika.

Kwa upande mtunzi wa kitabu hicho Kaduguda ambaye aliwahi kuwa katibu wa klabu ya Simba amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na wanachama na mashabiki wengi kutokuijua vyema historia ya klabu yao.

Amesema kwa mfumo wa kuyaandika mengi mazuri ya klabu ya Simba alioutumia kuna kila sababu kwa kizazi cha sasa na kijacho kuona mwanzo wa klabu hiyo mpaka ilivyo sasa na nini matarajio yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...