Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 11, 2014

RINO SALOON AND SPA YAWANG'ARISHA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT)


 
 Mshiriki Kutoka Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha Anneth Paul akipata Huduma ya kutengenezwa Nywele kutoka kwa Mmoja wa Wahudumu wa Saloon Nzuri na Ya kisasa kabisa ya Rino ambapo washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) walipoenda kupendezeshwa kwaajili ya Show ya Mchujo.
 Steven Mapunda mshiriki kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) akihudumiwa katika Saloon ya Rino iliyopo Msasani Karibu na Cape Town Fish Market
Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa ndani ya Saloon ya Kisasa Kabisa ya Rino iliyopo Msasani karibu na Cape Town Fish Market kwaajili ya kupatiwa huduma zote muhimu za saloon zikiwemo Kutengenezwa Nywele, Kucha, Uso na Nk kabla ya kwenda kushiriki kwenye Onyesho la Mchujo ambalo litafanyika jioni ya leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ambapo leo kuna washiriki wataaga Mashindano hayo.

Saloon ya Rino iliyopo Msasani karibu na Cape Town Fish Market ndio saloon pekee ambayo imewapedezesha Washiriki wote 20 wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kabla ya washiriki hao kwenda kushiriki kwenye Show ya Mchujo ambapo leo washiriki wawili wataaga Mashindano hayo ambao fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents itafanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane.

Kila wiki kutakuwa na Show ya mchujo ambapo washiriki wawili watatolewa katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo fainali yake itafanyika mwisho wa mwezi wa nane ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania na Washindi kumi bora watafanya filamu ya pamoja na Kunufaika na Filamu hiyo.

Ili kuweza kuwabakisha washiriki uwapendao unachotakiwa kufanya ni Kuwapigia kura washiriki kwa Kuandika ujumbe Mfupi wa Maneno kupitia Simu yako kwa Kuandika neno "TMT" halafu ikifuatiwa kwa namba ya Mshiriki na kutumwa kwenda 15678. MFANO: TMT00 tuma Kwenda 15678

Vilevile Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa katika Kituo Cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku na Kurudiwa Siku ya Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 Usiku.

Ili kuweza Kupata taarifa kuhusiana na Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) nenda kwenye simu yako ya Mkononi andika neno "TMT" halafu tuma kwenda 15678

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...