Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 11, 2014

MTAMBO WA GONGO KUZICHAPA NA Dula MBABE JUMAPILI YA AGOSTI 10,2014 CCM MWINJUMA MWANANYAMALA.

 Promotor wa mbambano wa ngumi za usiokuwa na ubingwa, Rashid Kipanga akiwatambulisha, Manenono Osward(Mtambo wa Gongo) kulia na Abdalah Pazi(Mudi Mbabe) wanaotarajia kuchuana Augosti 10,2014.Makubaliano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mwinjuma Dar es Salaam. 
 Na Mwandioshi Wetu.
BONDIA Mkongwe wa masumbwi, Maneno Osward maarufu kwa jina la “Mtambo wa gongo” jana amesaini rasmi kuzichapa na bondia chipukizi Abdalah Pazi maarufu kwa jina la “Dula Mbabe”.
Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) alisaini jana huku akimtahadhalisha mpinzani wake kuwa yeye hachagui umri,bali mtu yeyeto ambaye yuko tayari na vigezo vimezingatiwa vya Chama cha Ngumi nchini yeye yuko tayari muda wote.
Mtambo wa gongo wa Gongo alitamba kuwa kijana bondia chipukizi anayejiita Mudi Mbabe anataka kumbadilisha jina na kuwa Mudi mnyonge  na katika raundi 6 zilizopangwa hatafika mwisho.
Nae Abdalah Pazi bondia chipukizi alitamba yeye hataki ngojela atakachokifanya kwa anayejiita mkongwe wa masumbwi kitakuwa historia katika maisha yake kwani hatafika raundi ya nne.
Mwisho Mudi aliwataka wapenzi na mashabiki wa Ngumi kujitokeza kwa wingi hususani madereva bodaboda ambao ndio wafanyakazi wenzake wajitokeze kwa wingi kumshangilia atakavyomfanya vibaya Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) na kumbadilisha jina kuwa Mtungi wa maji.
Mbambano wa Maneno Osward(Mtambo wa Gongo) na Abdalah Pazi(Mudi Mbabe) umedhibitishwa na Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TBBC), Chaurembo Palasa ambaye aliwataka mabondia wasiwe chanzo cha fujo katika mpambano huo ikiwa ni kukuza na kuendeleza mchezo wa Ngumi nchini.
Mpambano huo utakuwa ni wa KG 78-Super middle weight utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam tarehe Augosti 10,2014 kuanzia saa kumi na mbili.
Wasanii watakaotoa burudani katika mbambano huo ni Kikosi cha Mizinga chini ya Uongozi wa Karapina,Sster P pamoja na wengine wengi.
Mgeni rasmi katika mbambano  huo ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.
 Mchezaji wa Nngumi, Maneno Osward(Mtambo wa Gongo) akisaini mkataba wa kupigana na Abadalah Pazi(Dula Mbabe) Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia
Mchezaji wa Nngumi, Abdalah Pazi(Mudi Mbabe) akisaini mkataba wa kupigana na Abadalah Pazi(Dula Mbabe) Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...