Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 11, 2014

JK. AMBARIKI RASMI JANUARY MAKAMBA URAIS 2015

Ampongeza kwa uwezo wake

amsifia kwa uwajibikaji wake

amtakia kila la heri kwenye safari yake. hii hapa sehemu ya maneno ya JK kama yalivyonaswa kutokea BUMBULIAlichokisema Rais ni hiki Kauli ya JK kama ilivyonaswa akiwa Bumbuli:

 ''January anafanya kazi nzuri ya Ubunge. Pia ananisaidia sana kwa kazi ya Wizara niliyompa. Unajua January alipogombea Ubunge alinificha. Nilikuwa nasikia kwa wenzake tu pale ofisini. 

Baadaye alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa. Nikamtakia heri. Kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka Kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli. Nimesikia anafikiria mambo makubwa. Hajaniambia. Mi Nimesikia tu. Namtakia kila la heri. 

Haya mambo anaamua Mungu. Wala hayalazimishwi. Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki. Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa. Mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani. Kama halijafika wakati wake haliwezi kutokea. 

Mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake. 2005 ikawa wakati wake nikapata. Na wewe usipopata sasa usiweke nongwa"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...