Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 28, 2014

NAIPONGEZA SERIKALI KUSITISHA AJIRA UHAMIAJI



Mgombea Uraisi Tucta Dismas Lyassa akijadiliana jambo na wakili wake Jebra Kambole. Picha na Mpigapicha Wetu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE



Ndugu zangu Watanzania


Asubuhi ya leo tarehe 28 Julai 2014 nilitoa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari nikiitaka Serikali kutolea ufafanuzi malalamiko yaliyojaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari. Asante Mungu kwamba Serikali imetolea majibu jambo hili kwa kusitiza ajira zote.

 Rejea taarifa yangu kwa vyombo vya habari niliyoitaka Serikali kutoa majibu katika suala hili asubuhi ya leo tarehe 28 Julai na nakala yake kutumwa katika ofisi mbalimbali za Serikali.


Nachukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuwa sikivu katika hili na huenda katika mengi yajayo, kama Rais Mtarajiwa wa Tucta baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 4-5 Dodoma, naahidi kushirikiana na Serikali hasa kama itakuwa sikivu.

Nahitaji kupatiwa majibu pia juu ya hatima ya mabaamedi wanaolazwa chumba kimoja zaidi ya kumi tena siyo katika vitanda, bali zaidi huwa wanalala chini; wanafanyakazi hadi usiku, wengine wanakoishi ni mbali na baa, hoteli nk.

Nahitaji kuona kero za walimu, wafanyakazi wa Serikali za Mitaa, madini, simu, kilimo, utafiti afya, mawasiliano, reli, bandari nk zinakomeshwa; Ni aibu hadi leo kuna walimu wanapoanza kazi  wanalala kwa walimu wakuu wakisubiri kupatiwa sehemu za kuishi, ni aibu hadi leo mwalimu anafanyakazi kazi miezi sita inapita hakuna mshahara anaolipwa…hatuwezi kwenda hivi, ni lazima majibu yapatikane.

Wafanyakazi wa Tanzania  tunapaswa kuimba nyimbo zingine, siyo za kero zile zile kila kukicha. Naamini yote yanawezekana, cha msingi ni kwa Serikali na waajiri kusimamia kwa haki mambo yote juu ya wafanyakazi. Hakuna lisilowezekana tukipigania haki.

Imetolewa leo Julai 28, 2014

                                   Na Dismas Lyassa                                  


(Mgombea Uraisi TUCTA) 
0754 49 8972/0712183282

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...