Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 20, 2014

Msondo, Sikinde uso kwa uso Iddi Mosi TCC Club

Magwiji wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra “Sikinde” siku ya Iddi Mosi watachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa Nani Mtani Jembe ni kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Id El Fitr na pia litaamua ni bendi ipi kali kati yao.Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga amesema pambano hilo litaanza saa nane alasiri hadi majogoo. 
 
Kapinga alisema bendi zote mbili ziko msituni kujiandaa na mpambano huo.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kulinda upinzani wao.
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera  alisema jana watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaisambaratisha Sikinde.
 
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera,  Eddo Sanga, Juma Katundu, Roman Mng’ande `Romario’  na Hassan Moshi.Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
 
“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Sikinde ni Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Abdala Hemba, Musemba Waminyugu.
 
Ramadhani Mapesa, Adofth Mbinga, Kelvin Mausi Mjusi Shemboza, Tonny Karama, Bonny Bass, Habibu Abass Jeff , Juma, Juma Choka, Mbaraka Othman, Hamisi Mirambo, Ali Yahaya, Yusuph Benard na Ali Jamwaka.Pambano imedhaminiwa na Konyagi na Saluti5.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...