Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 19, 2014

WANANCHI WATAKA STAMICO IPEWE NGUVU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI NCHINI.


indexWaunga mkono kauli ya Waziri wa Nishati na Madini,  Wataka wenye uwezo kuacha ubinafsi na ubepari, Wataka raslimali za madini ziwanufaishe Watanzania wote
Na. Issa Mtuwa – STAMICO
Wananchi wameiomba serikali kuhakikisha rasilimali za Madini zinawanufahisha Watanzania wote na sio wachache wenye uwezo. Kauli ambayo imewahi kutolewa siku za hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati walipotembelea katika banda la Shirika la Madini la Taifa STAMICO katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA) 2014, wananchi hao wamesema ili azma hiyo iweze kutimia ni vyema Serikali ikaijenga uwezo STAMICO kifedha na vitendea kazi ili iweze kutekeleza miradi ya uchorongaji na uchimbaji madini itakayowanufaisha wananchi. 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake alioambatana nao katika banda la STAMICO, Mkazi wa mkoa wa Mara, Bw. Joel M. Changarawe amesema katika kujenga uwezo wa kifedha wa Shirika hilo, Serikali haina budi kuendeleza azma yake ya kuikabidhi STAMICO migodi yote mikubwa ya Madini iweze kumiliki kwa niaba ya Watanzania na kuzalisha ili kuongeza tija kwa Taifa.

Jacqueline Aisaa akitoa maoni yake kuhusu sekta ya Madini wakati wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba 2014. Anae msikiliza ni Bw. Issa Mtuwa Afisa Uhusiano wa STAMICO.

“Nashauri Watanzania tuache ubinafsi na ubepari. Naishauri serikali Migodi yote ya Madini yenye RESERVE (akiba) kubwa imilikiwe na STAMICO kwa niaba ya Watanzania badala ya kukabidhi kwa Watanzania wachache wenye tamaa ya utajiri ambao wanamiliki vitalu vya madini kupitia migongo ya kampuni za kigeni” alisema Bwana Joel kwa kuandika kwenye kitabu maalum cha Maoni, ushauri na kero za Wananchi.

Naye Jacqueline Aisaa mkazi wa Masama-Moshi, ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya kwanza katika Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) alisema serikali iipe meno STAMICO ya usimamizi wa hisa zote za serikali kwenye migodi yote na usimamizi wa jumla katika sekta ya Madini ili Wananchi waweze kunufaika na raslimali hizo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...