Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 28, 2014

VIONGOZI WA CHUO NA HOSPITALI YA IMTU WATINGA MAHAKAMANI, DPP AWAONDOLEA MASHTAKA



 Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi 
 Wakipanda gari baada ya kusomewa mashitaka
 Wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka
 
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani. Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika kufundishia kwa Kampuni Coroner. 

 Vigogo hao ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo  saa 8:07  mchana.  Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey Lusemwa. 

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu washtakiwa wakiwa na nyadhifa  tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri, kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). 

 Magina alidai kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo baada ya kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka.
Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja. 


Hata hivyo, kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP akidai kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya kuendelea kuwashitaki. 

 Ahmed alidai kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu cha 91 kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaka. 

 Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa.

Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa. 
Alisema kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana ili wakasote mahabusu. 

 Viwanja vya mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa IMTU wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na lile. 

Kupitia magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...