Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 15, 2014

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA JIJINI DAR LEOGari ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likiwa eneo la Mwanyamala mapema leo mchana,ambapo moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba nzima na  mali zilizokuwemo,ambazo thamani yake haikujulikana mapema,tukio hilo limetokea maeneo ya Mwananyamala jirani na hospitali ya Mwananyamala.
Baadhi ya watu wakishuhudia tukio la Moto lililotokea mapema leo mchana,ambapo moto huo umeteketeza nyumba nzima na mali zilizokuwemo,ambazo thamani yake mpaka Globu ya jamii inaondoka eneo la tukio haikufahamika.
Baadhi ya Askari  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto kwenye moja ya chumba cha nyumba hiyo,Mashuhuda waliokuweo kwenye tukio hilo wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyokuwa imetokea kwenye moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo.
Majirani walijitokeza kuzima moto kwa kutumia ndoo kama uonavyo pichani 
Mabati yaliyobahatika kutetekea kwa moto yakitolewa nje.
 Askari  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto.
baadhi ya raia wema pia walijitokeza kusaidia kuuzima moto huo.Credit Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...