Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 11, 2014

Mtwara Festival

Taarifa kwa vyombo vya habari

The Mtwara FestivalWakazi wa Mtwara na Lindi kushuhudia fursa za Utalii na Uchumi kupitia Tamasha la Utamaduni la Mtwara.

10 Julai, 2014. Mtwara. Tamasha la Mkoa wa Mtwara, ‘Mtwara Festival’, linatarajia kufungua milango ya fursa kwa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi katika kuziona fursa kadhaa kwenye sekta ya Utalii na Uchumi.Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia mwezi Agosti 16 na 17 mwaka huu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona  ulipo Mtwara mjini. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Fursa Zimefunguka, Tuzitambue, Tujiandae, Tuzichangamkie.

Tamasha hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania Creative Industries Network (TACIN) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) huku likisaidiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumzia Tamasha hilo Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN, Anic Kashasha alisema kuwa mikoa hiyo inautajiri mkubwa katika utalii, uchumi na vivutio vingi mbalimbali.

"Mikoa hiyo ina utajiri mkubwa tena sana katika rasilimai zake mbalimbali kama vile fukwe nzuri na za kuvutia, utajiri mkubwa wa historia yake utamaduni na hata ubunifu wa aina mbalimbali hivyo matamasha kama haya yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utajiri huo," alisema Kashasha. Aliongeza kuwa, "Kwa sasa mikoa hiyo imeghunduliwa kuwa ina utajiri mkubwa wa gesi na hivyo kuna watu mbalimbali wameshaajiliwa ikiwa pamoja na kupatikana kwa fedha nyingi tayari kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na taifa zima kwa ujumla."

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu  ya TTB, Devota Mdachi alisema kuwa utalii umekuwa kwa kiasi kikubwa ukisaidia maendeleo ya uchumi wa nchi. Anasema kuwa katika tamasha hilo ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali za kiutamaduni, sanaa na nyinginezo ni nafasi kubwa ya kukuza utalii pia hasa utalii wa ndani au utalii wa kiutamadunia. "Ni nafasi kwao katika kutangaza mengi kuhusiana na masuala ya Utalii, hapa nchini au hata utai wa shughuli za kiutamaduni pia ni muhimu na hii ndio nafasi ya kipekee kwao na kwa wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono Tamasha hili la aina yake," alisema Mdachi.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Ofisa ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkuu wa Wilaya wa Mtwara na Mikindani Baraza la Wilaya la Mtwara Vijijini, Baraza la Biashara, KIlimo na Viwanda (TCCIA). Wengine ni Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Pride FM, Radio of Mtwara pamoja na Kampuni ya Mawasiliano ya Strictly Communications.

Kuhusu TACIN:
  
TACIN ni shirika lenye usajiri nchini lisilofungamana na upande wowote na lisilo la kiserikari, au la kibiashara, lenye makao yake jijini Dar es salaam.  Shilika hili huleta pamoja watanzania wenye uzalendo na nchi yao na wenye fani mbalimbali na uzowefu ambawo  wamejiridhisha na Creative Industries kama muendelezo muhimu unaohitaji uangalizo makini.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tacin.or.tz au info@tacin.co.tz

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...