Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 11, 2014

MSHIRIKI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) AZIMIA JUKWAANI MARA BAADA YA KUCHOMWA NA JUA LA UTOSI


Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambao wapo kwenye Maumivu ya kuchomwa na Jua la Utosi Wakimpa huduma ya Kwanza Mmoja wa Washiriki mwenzao ambae alipoteza fahamu jukwaani Hapo jana mara baada ya kuchomwa na Jua la Utosi na Kupelekea Kutolewa kwenye kinyanganyiro cha Kushindania Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane.Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam

Mara baada ya Safari ya Kuzisaka Nyota katika Kanda sita za Tanzania ambazo ni Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Pwani sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia katika hatua nyingine ya Washiriki kuwa chini ya Jua la Utosi huku mshiriki Mmoja wa TMT Kutoka Kanda ya Ziwa kuzimia Jukwaani mara baada ya kuunguzwa na jua la utosi kwenye Kinyanganyiro  cha Kuwania Kitita cha Shilingi Milioni 50 katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Mara Baada ya Mshiriki Huyo kuunguzwa na Jua la Utosi na kupoteza fahamu Jukwaani show ilisimama takribani Kwa muda wa Dakika 20 ili kuweza kuruhusu Mshiriki huyo kurudi Jukwaani ili zoezi zima la mchujo liweze kuendelea.

Shindano la TMT limekuwa likiwavutia Wapenzi na Watazamaji wengi wa kila rika kutokana na Utofauti wake, ubora wake pamoja na vipaji vinavyoendelea kuonyeshwa na washiriki wake katika Shindano hilo Kubwa kabisa na La Kwanza Kufanyika Afrika Mashariki na Kati.

Mara baada ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kuingia katika Jua La Utosi, Washiriki tisa waliweza kuchomwa na Jua la Utosi na Kupelekea Washiriki wawili kuondolewa katika Shindano hilo huku mshiriki mmoja akizidiwa hadi kupoteza fahamu jukwaani.

Jumamosi ya Kesho Katika Kipindi cha TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV Saa 4 Usiku washiriki tisa waliochomwa na jua la Utosi wataonyeshwa na hatimae watanzania, wapenzi na watazamaji wa Shindano hili kubwa Afrika Mashariki na Kati wataweza kujionea na kumfahamu mshiriki mmoja wapo kati ya wawili waliotolewa ambae alipoteza fahamu jukwaani kutokana na kuchomwa na Jua la Utosi na kupelekea Kutolewa kwenye kinyanganyiro hiko huku wengine Saba wakiponea Chupuchupu lakini hali zao zikiwa bado mbaya. 

Shindano la TMT limeanza kuvuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje ya Nchini kutokana na uzuri wake pamoja na Ubora.

Ili Kuweza Kumnusuru Mshiriki wako kutoka kwenye Maumivu ya Kuchomwa na Jua la Utosi unachotakiwa kufanya ni Kumpigia kura. Jinsi ya Kumpigia Kura Mshiriki wako ili kuwezesha kutokumbwa na kuchomwa na Jua la Utosi au kumnusuru kutoka kwenye maumivu ya jua la Utosi unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu tuma Kwenda 15678 kupitia simu yako ya Mkononi. MFANO: TMT00 tuma Kwenda 15678

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...