Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 21, 2014

WADAU WA MUZIKI WA INJILI IRINGA WAMCHOKA FLORA MBASHA WAMTAKA AIMBE MUZIKI WA BONGO FLEVER SIO INJILI TENA


Mwimbaji  wa  nyimbo za injili nchini Tanzania Flora  Mbasha
Flora  Mbasha akiwa na mumewe Emanuel Mbasha wakati wa  furaha ya  ndoa  yao

ZIKIWA  zimepita  siku  chache  toka  kumalizika kwa  sakata la mume wa Flora Mbasha kutuhumiwa  kumbaka shemeji yake na Flora Mbasha  kuhusishwa katika mchezo huo ,baadhi ya wadau wa mwimbaji  huyo mkoani Iringa  wamempa ushauri wa bure  mwimbaji huyo  kuwa kwa sasa ni vema akakaa kando na uimbaji wa nyimbo za injili na badala  yake  kujikita na uimbaji wa muziki wa bongo Flever 

Wakizungumza mtandao huu  wadau  hao Hosea Kalinga na Neema John   walisema  kuwa  heshima kubwa ambayo msanii  huyo alikuwa ameipata  imeporomoka kwa  kasi  kubwa  kufuatia matukio  mabaya yaliyoikumba  familia  yake na  hivyo hata kama waandaaji wa matamasha ya  injili  watamwalika  mwimbaji huyo ni wazi wanaweza  kuambulia patupu kutokana na kupotea ghafla katika mionyo ya  watu .

"Tulikuwa  tukimkubali  sana Flora Mbasha na Mumewe enzi  wakiimba pamoja  ila  kwa matukio haya ya kidunia ambayo yamewakuta   hakuna mpenzi  wa nyimbo za injili atakayempenda mwimbaji huyo na nyimbo zake ni  vema akatafuta soko la uimbaji katika miziki ya  dunia kama bongo Flever na sio injili tena"

Kuanza  kubezwa kwa  mwimbaji huyo kumekuja  kufuatia mgogolo wa ndoa yake ulioibuka kutokana na  sakata la mume  wake  kudaiwa  kumbaka shemeji yake  huyo  Flora  Mbasha akidaiwa kuwa na mahusiano na mmoja kati ya  wahubiri  wakubwa hapa nchini .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...