Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 18, 2014

MABINGWA DUNIANI GERMANY WATUA BERLIN NA KUPOKEWA NA MAELFU YA WATU


Fans greet the Germany teamGermany wamerudi Nyumbani kwao Berlin wakiwa na Kombe la Dunia mkononi baada kuwafunga Argentina 1-0 Juzi na kupokewa kwa shangwe kubwa na maelfu ya Wajerumani.That went well! Philipp Lahm and Thomas Muller pulled off a stunt on stage in Germany on Tuesday

Nahodha Philipp Lahm, akifuatiwa na Bastian Schweinsteiger, aliwaongoza Wachezaji wenzake kushuka toka kwenye Ndege.
Maelfu ya Wajerumani walikuwa wakiisubiri Timu yao katikati ya Jiji la Berlin, huko Brandenburg Gate, kwenye eneo linaloitwa Fan Mile, na Kikosi hicho kikiongozwa na Kocha Joachim Low kilikuwa kikizungushwa Mitaa ya Berlin wakiwa juu ya Basi la wazi na kuishia hapo Brandenburg Gate.
Having a ball: Christoph Kramer pretends to play the guitar as they entertain the huge crowd
Huku Mashabiki wakiimba: "Deutschland, Deutschland, Deutschland!", Kocha Low na Wachezaji wake walipokezana kuinua Kombe la Dunia juu na Basi kupita popole likilakiwa na kusindikizwa na Mashabiki kibao.
Boy band material? (from left) Hummels, Lahm, Durm, Kramer and Muller all get in on the guitar act
Huku wakiwa kwenye msafara huo, Wachezaji kadhaa wa Germany walichukua picha kwenye Simu zao na kuziposti moja kwa moja kwenye Twitter huku wakitoa maneno ya furaha.
Hii ni mara ya 4 kwa Germany kutwaa Kombe la Dunia na mara nyingine zilikuwa Miaka ya 1954, 1974 na 1990.
Pleased: Bastian Schweinsteiger and Lukas Podolski pose with the World Cup trophy in Berlin
Mbali ya sherehe hizo za Mjini Berlin, Kikosi hicho cha Germany kina Wachezaji wengi kutoka Bayern Munich na Klabu hiyo imeandaa sherehe maalum kwenye Mji wao Munich ili kuwapokea Wachezaji wao wa Kikosi hicho.

 Lahm akicheza pembeni mwa Thomas Mullerambaye kabeba kombe la Dunia  2014 waliloshinda huko Brazil siku ya Jumapili kwa kuwatungua Argentina bao 1-0, akiwa amelibeba mbele ya mamia ya mashabiki huko kwao Ujerumani leo hii.

 Podolski, Per Mertesacker, Mesut Ozil, Ron-Robert Zieler, Jerome Boateng na Sami Khedira
Mamia ya Mashabiki leo asubuhi huko Ujerumani wakiwasubiri Mabingwa wao Dunia


Wachezaji wakishusha mizigo yao

Wakipunga mikono kwa Mashabiki!!! Mesut Ozil, Ron-Robert Zieler, Erik Durm, Mats Hummels na Shkodran Mustafi

 Ozil, Benedikt Hoewedes na Per Mertesacker kwenye gari ya wazi na kombe lao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...