Madensa wa Kundi la Msanii wa kizazi kipya Tundaman, wakishambulia jukwaa.
Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, wakiwa katika vazi la jioni.
|
Mshindi wa nne , Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Elizabeth Perty kutoka mkoa wa Pwani akipita jukwaani na vazi la ubunifu. ******************************************** Na Mwandishi Wetu, Morogoror
MWANAFUNZI
wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ulinzi wa Jamii kutoka Chuo cha
Usimamizi wa Fedha ( IFM), Diana Laizer (21) amefanikiwa kunyakua taji
la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki baada ya kuwashinda wenzake 12
walioshiriki kuwani taji hilo mwaka 2013.
Mshindi
huyo ambaye pia ni malkia wa taji la Redd’s Miss Morogoro 2013 akiwa
amevalia namba sita ya ushiriki ,amefanikiwa kuchukua mikoba ya
mtangulizi wake Rose walifanikiwa kunyakua taji hilo juzi usiku katika
ukimbi wa Nashera Hoteli wa Mjini hapa baada ya kutangazwa na majaji wa
shindano hilo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Jaji
Mkuu , Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, mbali
na kumtangaza malkia wa Kanda ya Mashariki , alimtangaza pia mshiriki
kutoka mkoa wa Morogoro Sabra Islam (19) kushika nafasi ya pili katika
kinyang’anyiro hicho.
Sabra
aliingia kwenye shindano hilo baada ya kushika nafasi ya pili katika
shindano ya Redd’s Miss Morogoro 2013 ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo
Kikuu Mzumbe. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu huyo, mshindi wa tatu wa Redd’s
Miss Kanda ya Mashairiki ilitwaliwa na mrembo Janeth Awet ( 19) kutoka
Mkoa wa Lindi na nafasi ya nne ilinyakuliwa na mrembo Elizabeth Perty
(22) kutoka Mkoa wa Pwani. Makoye alisema kutokana na washiriki wa
kinyang’anyiro hizo Kanda ya Mshariki kuwa na warembo karibu wote wenye
sifa na vigezo,
Kamati
ya Miss Tanzania imeamua kuwachukua washiriki wanne kuingia katika
kambi ya shindano ya Miss Tanzania mwaka huu. Hata hivyo alimtaja
mwingine aliyeingia tano bora ni Ivon Stephen (22) kutoka Mkoa wa Mtwara
, ambapo wengi walioshiriki na mikoa yao katika mabano ni Zulfa Semboja
(19) ( Mtwara) na Pulkeriah Ndovi (21) ( Mtwara).
Wengine
ni Sophia Maganga (21), Lindi, Zainabu Shaaban (23) (Lindi), Lilian
Joseph (21) ,(Pwani ) Easther Albert (20) ( Pwani), Muzne Abduly ( 19)
na Ummy Mohamed (21) wote ni kutoka Mkoa wa Morogoro. Naye Mratibu wa
Shindano hilo, Alex Nikitas, aliwakabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza
sh: 600,000, Mshindi wa pili sh: 400,000 na mshindi wa tatu sh: 300,000 ,
ambapo mshindi wanne na watano walipatiwa sh: 200,000 kila mmoja na
wengine waliobakia kusawadiwa sh: 100,000 kila moja.
Katika
shindano hilo, Mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa ,
Mustafa Mkulo na pia kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo na Mbunge wa
Jimbo la Gairo , Ahmed Sabiby pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,
Jaji Frederick Werema ambapo pia mwanamuziki wa kizazi kipya Tunda Man
walitumbuiza likiwemo na kundi la sanaa la Wanne Star.
|
|
MC
katika shindano la kumpata malkia wa Taji la Redd's Miss Kanda ya
Mashariki Kaka Aidan Ricco ambaye ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss
Tanzania akielezea utaratibu wa kuwapata washindi watano. |
Mshiriki Zulfa Semboja kutoka mkoa wa Mtwara akionesha vazi la ubunifu mbele ya watazamaji
|
Washindi
wanne wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 wakisubiri Jaji Mkuu
kutaja majina yao katika nafasi ya ushindi kuanzia kwanza, pili , tatu
na ya nne. |
Mwanamuziki
wa Kike wa kizazi kipya, Keisha ( wa kwanza kulia) akipiga makofi
kufurahiamchuano wa warembo wa Redd's Miss Kanda Mashariki , Juni 29,
mwaka huu
Redd's
Miss Kanda ya Mashariki 2013 yenye taji kishwani akiwa kwenye picha ya
pamoja na washindi wenzake waliokuwa wameingia tano bora.
Redd's
Miss Kanda ya Mashariki 2013, Diana Laizer akifurahia kitita cha fedha
alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mustafa Mkulo baada
kutangazwa mshindi.
No comments:
Post a Comment