Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 27, 2010

CHANETA YAPATA MILION MBILI


Kaimu katibu mkuu wa CHANETA ROSE MKISI akipokea hundi ya shilingi milioni mbili kutoka LAPF

CHAMA cha NETIBOLI (CHANETA) kimepatiwa msaada wa fedha taslimu MILIONI MBILI na shirika la Pensheni LAPF kama msaada kwa timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini AFRIKA KUSINI mwezi ujao.

Wakati wa hafla ya kukabidhi hundi hiyo , Afisa masoko wa LAPF , REHEMA MKAMBA amesema msaada huo ni kusaidia timu hiyo kujiandaa na mashindano hayo yatakayoshirikisha mataifa mengi ya Afrika

Naye kaimu katibu mkuu wa CHANETA, ROSE MKISI amesema timu hiyo itaondoka nchini kwenda Afrika kusini SEPTEMBA TANO ambapo ni wachezaji KUMI na MBILI na viongozi WANNE ndio watakaokwenda nchini humo.NA janejohn5.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...