Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 24, 2010

MILIONI 800 ZATUMIKA KUTANGAZA UTALII LIGI YA UINGEREZA


Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza akifafanuwa jambo kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Aloyce Nzuki
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Aloyce Nzuki akizungumza na waandishi wa habari leo kulia ni Meneja Masoko wa bodi hiyo Geofrey Meena

Bodi ya Utalii Tanzania imeendelea kutumia mbinu mbalimbali za kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi, kadiri uwezo wa kifedha unavyoruhusu.

Kwa mara nyingine tena, Bodi ya Utalii imetumia michezo kutangaza vivutio vya utalii. Tofauti na huko nyuma ambako tulikuwa na timu za mpira kutoka nje ya nchi ambazo zilicheza hapa nyumbani, kwa mara ya kwanza sasa tumetumia michezo inayoendeshwa nje ya nchi kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia baadhi ya mashirika yake (hususani TANAPA na Ngorongoro), kwa uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania, tumenunua nafasi ya kutangaza kwenye viwanja vya nyumbani vya timu sita (6) zilizopo kwenye ligi kuu ya Uingereza, iliyoanza tarehe 14 Agosti, 2010 na itakamilika tarehe 22 mei, 2011.kwa galama ya milioni 800

Tanzania inakuwa ni nchi ya kwanza Afrika kuweka matangazo yake kwenye viwanja vya mpira katika ligi hii ya Uingereza.

Viwanja ambavyo Tanzania imeweka matangazo yake ni vile viwanja vya nyumbani vya timu sita zifuatazo:-


Kama ambavyo wengine mnafahamu, zipo timu 20 zinazocheza hii ligi kuu ya Uingereza, na kwamba kila timu inacheza na nyingine, nyumbani na ugenini. Sisi tumeweka matangazo yetu kwenye viwanja hivyo sita vya nyumbani, maana yake tutakuwa na jumla ya mechi 114, tangu kuanza kwa ligi hii tarehe 14 Agosti, 2010 hadi tarehe 22 Mei, 2011.

Tarehe 14 Agosti, 2010 siku ya kwanza ya ligi, timu tatu zilicheza kwenye viwanja vya nyumbani na matangazo yetu yalionekana. Timu hizo ni Blackburn Rovers, Sunderland, na Wolves.

Matangazo haya ni ya teknolojia ya “digital video” (yaani LED Perimeter Advertising) ambayo yataonekana kwenye kuta za kuzunguka uwanja. Matangazo haya ni ya sekunde 30 kila linaporushwa, na katika mechi moja tangazo hilo litarushwa si chini ya mara sita, kwa jumla ya dakika tatu kila mechi.

Kwa sekunde hizi 30, tumeandaa matangazo mafupi, hususan kuonesha vivutio vyetu maarufu, lakini mwisho wa kila tangazo kuna tovuti iayoitwa www.visit-tanzania.go.tz

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...