Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 18, 2010

RACHEL BALAMA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO


Anneth Kagenda na Rehema Maigala


MWANDISHI wa Habari wa gazeti la Dar Leo linalochapishwa na Kampuni ya Business Times Limited (BTL), Rachel Balama, amechukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kupitia Chama cha National Reconstuction Alliance Allance (NRA).BTL hutoa magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Dar Leo na Business Times.Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Rachel amesema ameamua kuwania kiti ili awatumikie wakazi wa jimbo hilo na kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabiri."Ubungo inakabiriwa na matatizo mengi, likiwamo tatizo sugu la maji, ninaimani nitakaposhinda, nitahakikisha nayazingatia hayo," amesema.Rachel ambaye ni Mkurugenzi wa Habari wana Takwimu Taifa wa chama hicho, ameahidi kutekeleza Ilani ya Chama chake kwa vitendo.Aidha amesema pia yeye akiwa mwanamke atahakikisha anawatetea wanawake wa Jimbo la Ubungo kwa kuwatafutia mikopo ambayo inariba ndogo ili kuweza kujikwamua na umaskini."Wanawake tunakabiliwa na matatizo mengi ndani ya jamii hivyo mimi nikiwa mwanamke mmoja wapo niliyejitosa kuwania kiti hiki ninauhakika nitashinda na kufanya mambo mengi ya kuleta maendeleo ndani ya jimbo langu," na kuongeza
"Ni kweli nilichukua fomu kwa ajili ya kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Ubungo ili kuwaletea wananchi wangu maendeleo makubwa huku wakinamama nikiakikisha wanapata mikopo kwa riba nafuu ili kujikwamua na umasikini kutokana na kwamba mimi ni mwanamke najua mahitaji wanayohitaji wanawake wenzangu''amesema Balama.Baadhi ya waliochukua fomu katika Jimbo hilo ni pamoja na Hawa Ng'humbi kupitia tiketi ya CCM, Julius Mtatiro CUF, Naomi Mabruk UPDP, Kamana Masoud UMD na Zabron Mazengo UDP.

Wengine ni Kambona Mwansasu TLP, Mark Kibogoyo SAU, Rashid Mawazo. NLP, Rajab Ismaili DP, Hamis Hamad APPT- maendeleo na John Mnyika CHADEMA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...