Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 16, 2010

KAMBI YA MISS TANZANIA YAANZA LEO
WALINZI WA KAMBI HIYO WAKIWA NJE YA GALI KULINDA USALAMA WA WAREMBO


Warembo waliofanikiwa kuingia Fainali ya Taifa ya Mashindano ya Urembo ya VODACOM MISS TANZANIA 2010, wanatarajia kuingia kambini siku ya kesho “jumatatu” tarehe 16 / 08 / 2010 katika hatua ya mwisho ya kinyang’anyiro cha kumsaka mlithi wa MIRIAM GERALD ambaye anamaliza muda wake wa kuwa Mrembo wa Taifa.

Wakiwa kambini warembo hawa watakuwa na ratiba mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kijamii na kutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya kitalii kama ifuatavyo:-

• Tarehe 17 / 08 / 2010 warembo watapewa semina maalumu na viongozi wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na kusaini mikataba kati yao na waandaaji.

• Tarehe 19 / 08 / 2010 waandishi wa habari wote watapata nafasi ya kuongea na washiriki na kupata maoni yao na jinsi walivyojiandaa katika kunyakuwa taji la VODACOM MISS TANZANIA 2010

• Mwishoni mwa wiki warembo wote wakiambatana na baadhi ya viongozi wa kamati watasafiri kwenda katika mikoa ya kanda ya kaskazini “KILIMANJARO: na “ARUSHA” kwa ajiri ya kutembelea vivutio vya utalii ili kuvitangaza na kuwahamasisha watanzania ili wajenge utamaduni wa kutembelea, kuvilinda na kuvithamini vivutio vyetu. Huu ni mpango tunaoshirikiana na taasisi za serikali yaani ,BODI YA UTALII, TANAPA na NGORONGORO CONCERVATION AREA AUTHORITY.

Huu ni mwaka wa pili taasisi yetu “Miss Tanzania” kushirikiana na taasisi za serikali kuhamasisha watanzania kuthamini na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu.

Tunategemea kwenda mbele zaidi kwa kuvitembelea vivutio vya kusini mwa Tanzania, SELOUS, RUAHA NATIONAL PARK, MIKUMI na UDIZUNGWA, katika siku za usoni.

Hashim Lundenga
Mkurugenzi.


Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye gari kuelekea kambini Dar es salaam leo walipowasili kwa ajili ya kambi hiyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...