Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 30, 2011

BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha


WASHINGTON, Marekani


BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha uzito baada ya pambano lake dhidi ya Lamont Peterson litakalofanyika Washington mwezi ujao kama Timothy Bradley atakataa kupigana naye.


Kwa mujibu wa Dail Mail Khan, ambaye ni bingwa wa dunia uzito wa Light-welter atataka kutwangana na Bradley katika mechi ya kuunganisha mataji.


Bondia mwenye miaka 28, Bradley nsiye anaonekana anaweza kutoa upinzani mkubwa kwa Khan katika uzito wao, lakini amekuwa akionesha kuwa hataki kupigana naye.


Khan mwenye miaka 24, anaamini kuwa kama

Bradley ataendelea kugoma kupigana hatakwua na uamuzi mwingine ataacha na mapambano ya light-welter na mikanda yake na kuhamia katika uzani wa welter ili kupata mechi kubwa.


Kama pambano dhidi ya Bradley litakuwepo kwangu nitabaki katika uzito nilio nao lakini kama halitakuwepo nitahamia katika uzito wa welter,"alisema Khan.


Alisema anataka kupigana na mabondia wapya na na lihi ndilo linamsukuma kwa sasa.


"Tutaona kitu gani kitatokea baada ya mechi hii na kama pambano dhidi ya Bradley litafanyika. kama sivyo nitapandisha uzito."


Khan atapigana Desemba 10 kwenye ukumbi wa Convention Center, Marekani dhidi ya Peterson atakayekuwa nyumbani.


Khan alisema: "Nina mtindo ambao watu wanapenda, kasi na ngumi kali na kweli anamini kuwa ingawa Peterson atakwua nyumbani nitaaungwa mkono zaidi kuliko yeye siku hiyo.


"Hawajapata pambano la kusisimua Washington kwa muda mrefu kwa hiyo itakwua kitu kizuri kwao. Kila wakati nimekuwa nikitamani kupigana katika miji tofauti ili watu kupata nafasi ya kuniona mimi jukwaani.


"Nilitaka kupigana na Bradley na nikaja kupiugana na Marcos Maidana na Zab Judah na kuwapiga wote."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...