Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 21, 2011

Ngumi kupigwa Desemba 18,MZALENDO PUBNa MWANDISHI WETU

WASANII mbali mbali hapa nchini wanatarajiwa kutoa burudani katika pambano la mchezo wa ngumi lisilo na ubingwa litakalowakutanisha bondia, Mada Maugo na mpinzani wake Suleimani Saidi 'Toll' Desemba 18 mwaka huu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama JIjini Dar es Salaam.

Akizungumza na kona hii ya burudani Raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa hapa nchini (PST) Emanuel Mlundwa alisema, maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.


Aliwataja wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa (Halidi Chuma)pamoja na msanii wa mziki wa bongo fleva Mwana FA (Hamisi Mwinjuma).

Alisema licha ya kuwepo kwa burudani hizo vile vile atakuwepo kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D kwa ajili ya kutoa mafunzo kupitia Dvd pamoja na kuzisambaza.

Aliwataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo haupewi kipaombele watahakikisha wanasonga mbele katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru.

aidha katika mapambano ya ngumi ya utangulizi mabondia Yohana Miyayusho na Shadrack Juma, Doto Kipacha atazidunda na Saidi Muhidini na kwa upande wa mchezo wa Kick Boxing ambao utatuwakilisha kimataifa Tanzania Muaythai Academy of Combat watawaletea mpambano kwa mara ya kwanza nchini kati ya bondia Emanuel Shija kutoka Tanzania na Munyeshyaka Vincent kutoka Rwanda Mpambano huo utakuwa wa kimataifa kutokana na ushiriki wake wa nchi hizo mbili nchini zitakuwa zikipeperusha bendera zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...