Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 10, 2011

MPAMBANO WA MTOTO WA BAKHRESA NA WAPIGA PICHA ZA HABARI WALIOKUWA WAKIPIGWA KWA HELMETI ILI WASIMPIGE PICHA YA AJALI


Jamal Bakhresa akitumia helmeti kuwapiga nayo waandishi wa habari waliodaiwa kumpiga picha yeye na mwendesha pikipiki mwenzake walipogongana katika Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana. Anayejaribu kumzuia ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda ambaye alipigwa na helmeti hiyo kichwani. Pembeni ni Cathbert Kajuna ambaye ni mwandishi wa gazeti la Kitangoma linalomilikiwa na Clouds Media ya jijini Dar es Salaam na pia ni mmiliki wa blog hii alikuwa akijaribu kumuamulia ugomvi.
Hapa Cathbert Kajuna aliyekuwa akijaribu kumdhibiti Jamal Bakhresa ili kumnyang'anya helmeti aliyokuwa akitumia kumpigia mwandishi Mwaikenda. Hali hiyo iliweza kuleta mtafaruku mkubwa.
Hapa waandishi wapiga picha Cathbert Kajuna na Richard Mwaikenda walikuwa wakimfokea Jamal kwa kitendo chake cha kuwaingilia wakati wakiwa kazini. Vitendo kama hivi vya kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao vimekuwa vikitokea mara wa mara ambapo vimekuwa vikiwasababishia hasara ya mali zao na vifaa kupoteza vifaa vya kazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...