Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 9, 2011

Michuano ya SHIMIWI Yapamba Moto Tanga, Wahisani wa Mashindano hayo Wapewa Tuzo


Wachezaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria (Tumesheria Sports Club) wakiwa wameshika bango wakati wa maandamano ya uzinduzi wa michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Tanga.

Mkurugenzi wa Kampuni ya ZH POPPE Bw. Zacharia Hans Poppe akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw. Ibrahim Msengi mara baada ya kutunukiwa Tuzo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fenela Mukangala.
Mkuregenzi wa Kampuni ya DP Shapriya Bw.Dipak Kotak akiangalia Tuzo aliyotukiwa kwa kutoa mchango wa kufanikisha mashindano ya SHIMIWI, mwingine mwenye tuzo ni mwakilishi wa Kampuni ya Twiga Cement Bw. Mahmoud
Timu ya wavuta kamba ya Mambo ya Mambo ya Nje Kimataifa ikihangaika kujinasua ilipochuana na HAZINA ambapo katika mchezo huo timu ya HAZINA iliibuka mshindi
Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba wanawake ya TUMESHERIA Sports Club wakiwa pamoja na Katibu Msaidizi wa Tume Bw. Adam Mambi (wa kwanza kulia) mara baada ya kutangazwa washindi dhidi ya Wizara ya Afrika Mashariki
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dr. Fenela Mukangara akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mkoani Tanga.
http://fullshangwe.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...