Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 23, 2011

WANAHABARI WAHUDHURIA KILINIKI YA TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 DICC


Mkurugenzi wa Mashindano katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw. Saad Kawemba akizungumza wakati wa kliniki ya mashindano ya Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA yanayojulikana kama (TUSKER CACAFA CHALLENGE CUP 2011) inayofanyika kuanzia asubuhi hii kwenye ukumbi wa mikutano wa DICC PPF Tower jijini Dar es salaam, ambapo waandishi wa habari watakaoandika habari za mashindano hayo kutoka nchi mbalimbali ukanda wa Afrika Mashariki wanahudhuria na kupata maelezo mbalimbali .
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Bw. Nicholas Musonye akitoa mada katika Kliniki hiyo, mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Bw. Nicholas Musonye na Meneja wa bia ya Tusker inayozalishwa na kampuni ya Serengeti Breweriers Ritah Mchaki wakifuatilia jambo, wakati Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF Saad Kawemba alipokuwa akitoa mada yake na kukaribisha waandishi mbalimbali waliokuja nchini kwa ajili ya kuandika habari za mashindano ya TUSKER CACAFA CHALLENGE CUP 2011.
Washiriki wa Kliniki hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyokuwa yakitolewa na watoa mada katika kliniki hiyo.
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini mkubwa mambo mbalimbali yaliyojiri katika kiliniki hiyo.
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini mkubwa mambo mbalimbali yaliyojiri katika kiliniki hiyo.
zaidi tembelea http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...