Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 30, 2011

SERENGETI BREWERIES ANZISHENI VIWANDA NJE YA NCHI, PINDA


Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda cha SBL, Mhe. Pinda aisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbali mbali waliokuwepo katika uzinduzi huo.
Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kati) akipiga makofi mar baada ya ufunguzi wa kiwanda hicho, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa EABL, Seni Adetu, na kulia kwake ni Waziri wa Manispaa ya Nairobi, Bw. Njeru Githae ambaye alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu Raila Odinga wa Kenya na wageni wengine waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
---
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameitaka kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd. (SBL)nchini kuanzisha viwanda katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kupanua soko la bia hiyo na kupata faida zaidi.

Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha kisasa cha Serengeti mjini Moshi leo (Jumanne Nov. 29, 2011) Mhe. Pinda alisema Kampuni hiyo lazima ijipanue kama vile wafanyabiashara wengine wa nje wanavyowekeza nchini.

“Kwa vile bidhaa yenu inapendwa hata soko la nje, anzisheni viwanda Burundi au Uganda… wenzetu wa nje wanafanya vivyo hivyo na kuwekeza hapa nchini,” alisema.

Kiwanda cha Serengeti Moshi, ambacho kimejengwa kwa ubia na Kampuni ya Bia ya East African Breweries Ltd. (EABL) ya Kenya ni cha tatu nchini. Vingine viwili vipo Dar es Salaam na Mwanza.

Bia ya Serengeti ilipata tuzo kwa kuwa ya kwanza katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Ireland hivi karibuni.

Waziri Mkuu pia alisema ataitisha kikao kitakachomjumuisha Waziri wa Kilimo na Chakula na wawakilishi wa Serengeti Breweries ili kuhakikisha namna bora ya kupata kwa uhakika mali ghafi muhimu ya kutengeneza bia, mtama.

Alisema mtama unaweza ukawa biashara nzuri kwa wakulima kwa kuwa Serengeti Breweries wanaununua kwa Sh. 600 kwa kilo moja ikilinganishwa na bei ya mahindi ambayo ni wastani wa Sh. 350 kwa kilo.

“Kuzalisha mtama ni gharama nafuu zaidi kuliko mahindi na kwamba zao hilo linastahamili ukame. Tukutane na Wairi wa Kilimo kuona namna ya kupata zao hili nchini kwa uhakika zaidi,” aliongeza.

Serengeti Breweries inahitaji tani 18,000 za mtama kwa mwaka, lakini upatijanaji wake hauna uhakika, Waziri Mkuu aliambiwa.

Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Manispaa ya Nairobi, Bw. Njeru Githae ambaye alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu Raila Odinga wa Kenya; Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bibi Diane Corner na Mtendaji Mkuu wa EABL, Bw. Seni Adetu.

Mapema, kwenye Ikulu ndogo, mara baada ya kuwasili Moshi, Mhe. Pinda alisomewa taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Leonidas Gama na kusifu jitihada za mkoa za kujietea maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...