Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 9, 2011

Dk. SLAA APANDISHWA KIZIMBANI


Katibu mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa akishuka katika karandinga leo baada ya kufikishwa katika mahakama kuu ya mkoa wa Arusha kusomewa mashitaka matatu yanayomkabili yeye binafsi likiwemo la kumdhalilisha Rais,Slaa alipandishwa kizimbani pamoja na mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu na washitakiwa wengine 25 ambao wanakabiliwa na mashitaka mawili ya likiwemo la kufanya mkusanyiko usio na kibali wa mkesha usiku wa jana pamoja na kukaidi agizo la
polisi lililowataka kutawanyika katika uwanja wa NMCP

Wengine waliofikishwa mahakamani pamoja na Dk.Slaa kuhusu mashitaka hayo ni Tundu Lissu,David Godfrey (18), Ally Hussein (20), Frank Chami (24), Stella Mushi (21), Francis Smweli (20), Paulo Meena (18), Beatrice John (28), Matei Thobias (38), Davies Sedeka (29) na Wilson Andrea (24).
Wengine ni Richad Urasa (27), Abubakar Mrema (25), Peter Davis (14), Proches Blacy (36), John Msaki (53), Stephano Swai (33), Mohamed Mhoji (21),Titus Urio (30), Nelson Kimario (23), Meshack Beture (23) na Jimmy Evarist (22)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...