Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, November 20, 2011

SERENGETI YAANDAA HAFLA KWA WANAHABARI KUPATA MAONI KABLA YA MASHINDANO YATUSKER CECAFA CHALLENGE CUP


Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) Richard Wells akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi wa michezo katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika hoteli ya JB Bellmonte jijini Dar es salaam mchana wa leo. Lengo la Mazungumzo hayo ilikuwa ni kujadili mambo mbalimbali na kupata mchango wa mawazo kwa wanahabari kabla ya kufanyika kwa mashindano ya TUSKER SECAFA CHALLENGE CUP 2011yatakayoanza hivi karibuni jijini Dar es salaam. (PICHA ZOTE NA MOHAMED MAMBO)
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Ephraima Mafuru akimkaribisha mkurugenzi wa kampuni hiyo ili kutoa maneno machache katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Tanzania TFF Angetile Osiah naye alipata muda wa kuongea kidogo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akizungumza katika hafla hiyo katika hoteli ya JB Bellmonte jijini Dar es salaam.
Wanahabari wakijipakulia misosi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya JB Bellmonte jijini Dar es salaam leo.
Umakini ulikuwa muhimu hapa kama wanavyoonekana katika picha wakimsikiliza Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto hayupo pichani , kutoka kulia ni Richard Wells Mkurugenzi wa (SBL), Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko (SBL).
Kutoka kulia Juma Pinto Mwenyekiti wa TASWA, Richard Wells Mkurugenzi wa (SBL), Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko (SBL).
Mkurugenzi wa SBL Richard Wells akijadili jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda katikati na Meneja wa Mahusiano ya Jamii Nandi Mwiyombela kushoto.
Mkurugenzi wa Sports Radio FM Abdallah Majura akijadiliana jambo na waandishi wa habari wenzake katika hafla hiyo, aliyenimama nyuma ya Abdallah Majura ni Meneja Mawasiliano Serengeti Breweriers Imani Lwinga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...