Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 21, 2011

WATANZANIA WANAOISHI UJERUMANI ! WAANZA KWA KASI! KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA


Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanaanza kusherekea sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara,
kwa vishindo na vilivyochanganyika na shangwe zisizo mfano, kuwa siku ya Jumamosi 3 -12-2011 Uzinduzi wa.
sherehe hizo utaanzia mjini M√ľnchen,katika mtaa wa Siebold Str,11,majira ya saa 10 alhasiri, na usiku bendi maarufu ya
muziki wa dansi Ngoma Africa Band wanatarajiwa kutumbuiza katika sherehe hizo za kihistoria.
Huko Mjini Berlin ,ambako ndio makao makuu ya ujerumani,kuanzia siku ya 9.Dec.2011 mji huo utatingishika na
sherehe hizo siku ya JUMAMOSI 10 Dec 2011 ndio siku ambayo watanzania na marafiki wa watanzania,wakiwemo
wahisani ,watajimwaga uwanjani kusherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, bendi ya muziki kikosi kazi cha
NGOMA AFRICA BAND aka FFU ambacho kinatazamiwa kumwaga burudani ya muziki kitakuwepo uwanjani,
katika usiku usiokucha, Ngoma Africa band pia wanatamba na CD mpya ya "Shangwe 50 Uhuru Anniversary",
ambayo imeshaanza kutingisha katika vituo mbali mbali vya Redio ndani na nje ya Tanzania,unaweza kusikiliza pia hapa
WATANZANIA WANAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI ! Kama wahenga wanavyosema
CHEREKO ! CHEREKO ! NA MWENYE MWANA !

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...