Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 30, 2011

DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko

LONDON,

DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko kujadili uwezekano wa kufanyika pambano kati yao Machi mwakani.

Mpiganaji huyo wa London alitangaza kustaafu ngumi Oktoba mwaka huu lakini amesema kuwa yuko tayari kupigana tena kama atapata nafasi ya kurudiana baada ya kupoteza pambano lake Julai dhidi ya Wladimir Klitschko ambaye ni kaka wa Vitali.

Haye mchezo huo alisema: " Sijaona mkataba lakini kuna mazungumzo yanayoendelea.

"Nilisema kabla kabla ya kustaafu ningependa pambano hilo na kuna tarehe katika Machi ambayo imekuwa ikizungumziwa."

Mabondia hao wazaliwa wa Ukraine wamekuwa wakisema kwua mabalkuanalino yanafanyika ili kuwepo pambano la kuwania ubingwa wa WBC unaoshikiliwa na Vitali, baada ya Haye kupoteza pambano ambalo lilifanya apokwe ubingwa wa IBF/WBO dhidi ya Wladimir mjini Hamburg Julai mwaka huu.

Haye mwenyewe alisema amestaafu ngumi lakini yuko tayari kurejea ulingoni kama atajitokeza mmoja kati ya wanamasumbwi wa familia ya Klitschko.

Kumekuwa na mazungumzo kuwa huenda pambano hilo likafanyike Machi mwakani katika mji wa Dusseldorf Ujerumani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...