Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 17, 2013

BI KIDUDE HATUNAE TENA DUNIANI


HABARI zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinaeleza kuwa mwimbaji mahirina mkongwe  wa miondoko ya  taarab, Fatma Baraka , ama Bi Kidude amefariki dunia mchana huu.
Kwa mujibu wa Mjukuu wa marehemu, Fatuma Kidude amesema kuwa bibi yake amefariki nyumbani kwa mtoto wa kaka yake maeneo ya Bububu, mjini Zanzibar.
Fatma ambaye naye pia ni mwimbaji wa kundi la Gusa Gusa la Dar es Salaam ameongeza kuwa bado taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika lakini mwili wa marehemu unahamishwa  nyumbani kwake Raha Leo.

Bi Kidude alianza kusumbuliwa na maradhi  mwaka jana, lakini baadaye akapata ahueni na kufanya mahojiano hadi na vyombo vya habari, lakini ghafla mambo yakabadilika tena na kulazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam.
Baada ya matibabu akaambiwa asiimbe tena na tangu Machi mwaka jana hajapanda jukwani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...