Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 23, 2013

TASWA FC, TASWA QUEENS, KUCHEZA KIBITI JUMATANO



Kikosi cha Taswa Fc.

Kikosi cha Taswa Queens.
*************************************
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) na timu ya netboli (Taswa Queens) itaondoka jijini Jumatano alfajiri  kwenda Kibiti, mkoa wa Pwni kwa ajili ya mechi maalum ya kirafiki.

Mechi hiyo imepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Samora imeandaliwa kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa karibu baina ya waandishi wa habari za michezo na walimu wa wilaya hiyo katika kuendeleza sekta hiyo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa mechi ya kwanza siku hiyo itakuwa kati ya Taswa Queens na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 9.00 ambapo mechi ya pili itakuwa kati ya Taswa FC na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 10.00 jioni.

Majuto alisema kuwa mbali ya kuanzisha uhusiano na kupromoti michezo katika wilaya hiyo, mechi hizo pia zitakuwa sehemu ya maandalizi ya Taswa FC na Taswa Queens kwa ajili ya ziara ya kimichezo mkoani Arusha na Tanga mwezi ujao.

“Maandalizi ya safari yamekamilika na tunawaomba wachezaji wazingatie muda wa kufika ili tuweze kuondoka kwa mujibu wa ratiba yetu, lengo ni kuwahi kufika na kumaliza mapema na kuendelea na ratiba nyingine kwa mujibu wa wenyeji wetu,” alisema Majuto.

Alisema kuwa timu zao zote zimejiandaa kwa ushindi katika mechi hizo ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na maandalizi. Taswa FC haijapoteza hata mechi moja tokea kuanza kwa mwaka huu. Timu zote mbili zilitoa vipigo kwa timu ya Kiliflora ya Arusha kwa mabao 4-1 kwa upande wa soka na mabao 28-8 kwa upande wa netiboli.

Mratibu wa mechi hiyo, mwalimu Paul Nyoni amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na wanawasubiri kwa hamu waandishi wa habari. Nyoni alisema kuwa wamewaandalia mapokezi mazuri kwa waandishi na wanaamini mechi hizo mbili zitakuwa na mvuto na ushindani mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...