Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, April 13, 2013

VODA COM TANZANIA NI MKOMBOZI WA WATANZANIAKAMPUNI ya Voda com nchini hivi karibuni ilianzisha huduma ya kipekee ambayo ilikuwa inamuwezesha mtumiaji wa mtandao wa VODACOM kununua muda wa maongezi wa mitandao mingine nchini kwa kutumia huduma za M PESA.

Huduma hii ni mapinduzi makubwa kwenye mtandao wa VODACOM ambayo mbali ya kukuza huduma yake imeweza kuvuka mipaka na kusaidia wateja wa mitandao mingine

Kampuni ya Vodacom ambayo kwa sasa inatamba na huduma yake bora ya M-PESA iliyojizolea umaarufu mkubwa nchini kupitia huduma hiyo
VODACOM ambayo siku zote imekuwa karibi sana na jamii hivi karibuni ilikuwa na huduma nyingine nzuri sana ambayo ilikuwa inamuwezesha mteja wa M-PESA Kununua vocha ya mitandao mingine nchini hii ni huduma iliweza kuwa ondolea adha wateja pindi wanapotaka kuwanunulia muda wa maongezi wenzi wao ambao wapo katika mitandao mingine ili kufanya hivyo mteja wa MPESA alitakiwa kuingia kwene menu ya Mpesa na kufuata taratibu kama afanyavyo anapotaka kununua LUKU au huduma nyingine ila hii ni kununua muda wa maongezi wa mtandao mwingine alipaswa kuinginza namba 484848 kama namba ya kampuni na kisha kuingiza namba ya simu ya mtu anayetaka kumtumia mda wa maongezi kwa mtandao wowote ule nchini kama namba ya kumbukumbu

Hakika huduma hii ni nzuri na inarahisisha maisha na inawezesha watumiaji wa mtandao wa voda com kuwa nunulia wenzi wa

o muda wa maongezi pasipo kujali wana tumia mtandao gani

Haya ni mapinduzi makubwa ya kutechnologia nchini na yanapaswa kuungwa mkono na kupewa Baraka zote
Kinacho nishangaza mpaka sasa nikiwa kama mwana habari ni kuwa mbali na huduma hii kuwa nzuri na kuwaaidia watanzania hususani watumiaji wa mpesa huduma hii sijasikia kutangazwa  ili watanzania wote waijue na kama nionavyo mimi ambaye nimeshaitumia na kujua uzuri wake naona ni bora itangazwe zaidi ili jamii ijue na kunufaika nayo.
Mbali na uzuri wake na kurahisisha maisha kinacho nistajaabisha kuwa katika siku kama mbili zilizopita nimekuwa nikijaribu kutumia huduma hiyo na imekuwa haipatikani na jamaa zangu ambao wote tumekua tukitumia huduma hiyo kwa pamoja tunajiuliza kulikoni nini kimetokea hadi huduma huu nzuri ikasimama

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...