Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 25, 2013

Sikinde kutambulisha mpya wakielekea Mbeya kwenye Mei Day


Waimbaji wa Mlimani Park 'Sikinde' Hassani Kunyata, Abdallah Hemba na Hassani Bitchuka 'Stereo' watakaotoa burudani kwa wakazi wa jijini la Mbeya na vitiongoji vyake kuanzia kesho wakienda kwenye Mei Day

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' inatarajiwa kutambulisha nyimbo zake mpya katika miji kadhaa wakati wakielekea Mbeya katika sherehe za Mei Day.
Sikinde imealikwa kutumbuiza katika sherehe hizo ambazo kitaifa zitafanyikia kwenye mkoa huo wa Mbeya wiki ijayo.
Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo alisema wakati wakiwa njiani kuelekea Mbeya watafanya maonyesho kadhaa katika maeneo mbalimbali na nje na ndani ya mkoa huo.
Milambo alisema maonyesho hayo yataanza kesho Ijumaa watakapotambulisha nyimbo zao kwenye ukunbi wa Comfort Chamazi, kabla ya Jumamosi kuwa City Pub uliopo Mwanjelwa.

Sikinde itaendeleza makamuzi yake siku ya Jumapili eneo la Tunduma kabla ya siku ya Mei Mosi kutumbuiza kwenye sherehe za Mei Daya asubuhi kwenye uwanja wa Sokoine kabla ya usiku kufanya vitu vyao ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini humo.
"Siku ya Mei Mosi tukishatoka kutumbuiza uwanja wa Sokoine tutafanya onyesho katika ukumbi maarufu mjini humo kisha kuanza safari ya kurejea Dar kuendelea na mengine," alisema.
Milambo anasema katika maonyesho yote watatambulisha nyimbo zao wanazoziandaa kwa ajili ya albamu mpya kama 'Jinamizi la Talaka', 'Kuvunjika kwa Dole Gumba', 'Nundule' na nyingine.
"Pia tutawapa burudani mashabiki kwa kuwakumbusha vibao vyetui vya zamani vilivyotufanya Sikinde kutambuliwa kama 'Mabingwa wa Muziki wa Dansi Tanzania," alisema Milambo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...