Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 30, 2013

WESTERN UNION YAKABIDHI ZAWADI KWA WSHINDI WA PROMOSHENI YA UEFA


  Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa (wa pili kushoto) akikabidhi tiketi ya kwenda na kurudi Uholanzi kwa Quraish Omari Shindo mmoja wa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Meneja wa Benki ya Posta Tanzania  Tawi la Samora), Deo Kayega.
 Meneja wa Tawi la Samora wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Deo Kayega (wa tatu kushoto) akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa Nicetus Joseph, mmoja wa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa.
 Meneja Masoko wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi (kushoto) akionyesha mfano wa tiketi ya kwenda na kurudi Uholanzi atakayopewa mshindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kushoto kwake ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa.
Mkurugenzi ya Kampuni ya twenty4 Brand Communications, Monte Bilal Ikoa (kushoto) akizungumza katika hafla ambayo Western Union walikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...