Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, April 27, 2013

MSAMA ATINGA BUNGENI


waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na uwezeshaji,Dk Mary Nagu,(kushoto)akimuelekeza mambo ya uwekezaji wa ndani Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama,Alex Msama,walipokutana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma  ambapo vikao vya bunge la bajeti vinaendelea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na uratibu Bunge,Wiliam Lukukuvi (kulia)akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama,Alex Msama,watatu kutoka kulia,walipokutana nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma,wengine ni Michael Laiza Longido(CCM) Athumani Mfutakamba,Igalula(CCM)na, John Chiligati,Manyoni mashariki(CCM).

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA)Freeman  Mbowe,(kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama,Alex Msama,walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma mara bada ya kuahirishwa kwa kikao cha kujadili bajeti ya wizara ya maji
Wabunge wapambanaji kutoka chama cha Mapinduzi CCM,Kangi Lugola, Mbunge wa Mwibara,(kulia)na Deo Filikunjombe, wa Jimbo la Ludewa, wakifurahia uwasilishaji wa hoja zao za kuwatetea wananchi wao bungeni katika mkutano wa bajeti unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof,Jumanne Maghembe,(katikati) na Naibu wake Dk,Binirith Mahenge, watatu kushoto,na Abdulsalami Amer, Mbunge wa Mikumi,wakiingia kuhitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yao ambao hata hivyo ulikwama kupitishwa kutokana na wabunge kutounga mkono kutokana na uchache wa fedha zilizotengwa,mjadala huo unaendelea leo bungeni mjin dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki,(kulia)akishauriana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Bunge, Wiliam Lukuvi(kushoto)ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma,katikati ni Mbunge wa Iramba Magharibi(CCM)Mwigulu Nchemba.
Waziri wa Maliasil na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo,Amos Makala,(kushoto)akifurahia mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama,ambae ni mpambanaji dhidi ya maharamia wezi  wa kazi za wasanii wa muziki hapa nchini,walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma..

Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai,(kulia) akitafakari mambo ya bajeti ya Wizara ya maji na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama, Alex Msama,mara baadaya kukwama kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...