Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 18, 2013

HUKUMU YA PONDA YAAHIRISHWA HADI MEI 9


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea  kupanda basi la magereza baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano ya kula njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T uliopo Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Shs milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza. (Picha na Habari Mseto Blog) 
 Saleh Mkadamu akipanda basi kuelekea mahabusu
 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
 Ulinzi mkali kila kona ya mahakama
 Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
 Msafara wa magari ya Polisi wakisindikiza gari la magereza lililomchukua Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakati wakielekea mahabusu baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa leo hadi Mei 9.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...