Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 18, 2013

NGUMI KUPIGWA CHALINZE


Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar
Mabondia Mwaite juma,cosmas kibuga na shabani kaoneka ni baadhi ya mabondia wa dar es salaam watakaokwenda chalinze kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa chalize.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia machipukizi ya Bigright Promotion, imaeandaa pambano hilo  litakalofanyika mei 20 ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimchezo ikiwemo chalinze.
Tumeamua kufanya chalinze kwa sababu tunataka chalinze iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa dar na wakali wa chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu. ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi Mkwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa  Chalinze bwilingu bw Nasser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka dar es salaam kwenda kushangilia na kurudi.
wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wangumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo 
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya ma bondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali
 
 
ibrahim kamwe

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...