Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 25, 2013

Msondo Ngoma yapeleka mpya Magereza


Waimbaji nyota wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede 'Kamchape' na Juma Katundu 'JK wa Msondo'
BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma,  inatarajiwa kuwapelekea burudani mashabiki wao wa maeneo ya Mtoni kwa Aziz Ali na Magereza Ukonga.
Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila 'Super D' aliiambia MICHARAZO kuwa, bendi yao imeongeza ratiba ya kutoa burudani wiki hii kwa mashabiki wa maeneo hayo.
Alisema Msondo inayojiandaa kupakua albamu mpya ya 'Suluhu' leo itatoa burudani Mtoni kwa Aziz Ali kabla ya kesho kwenda Magereza Ukonga.
"Jumatano na Alhamisi tutakuwa tukitoa burudani katika maeno hayo, na Ijumaa hadi Jumapili ratiba inabaki kama ilivyo," alisema.
Alisema kwa kuwakumbusha mashabiki wao, Ijumaa hufanya vitu vyao Leaders na Jumamosi  huwa TCC Chang'ombe na Jumapili watavuka bahari hadi Kigamboni.
"Jumapili tutakuwa G-Five Kigamboni, ambapo Msondo itapiga nyimbo za zamani na mpya zilizoifanya iitwe Baba ya Muziki," alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...